LEONARDO DICAPRIO: MWIGIZAJI ANAYEPENDA KIFO.LEONARDO DICAPRIO ni mmoja kati ya actors wanaofanya  vizuri Hollywood , Leo kaigiza movies chache sana ila ana mafanikio makubwa kuliko hata waigizaji wenye movies nyingi, Leo kaigiza movies 36 tu hadi sasa na kupitia movies hizo amefanikiwa kuwa nominated kwenye tuzo za oscar mara 5 na kufanikiwa kushinda 1 mwaka 2016 kupitia movie ya The Revenant.Leo ni mmoja kati ya waigizaji wanaopenda kufa katika movies walizoigiza hadi sasa kafa zaidi ya mara 10,Kifo chake kilichowaumiza wengi ni katika movie ya Titanic aliyoigiza kama Jack...Lets check movies nyingine alizopoteza maisha akiwa kama main character au supporting actor.


Leo anakufa katika movie ya THE QUICK AND THE DEAD, katik movie hii Leo kaigiza kama Fee kijana ambaye anajitoa muhanga kuingia katika mashindano ya kupigana kwa bunduki (Gun Fighting contest) nia ni kumvutia kiongozi mmoja mkatili wa mji ambaye Fee anahisi kuwa huyo mzee anaweza kuwa ni dingi yake.
ANAKUFAJE? : ili kupata heshima ya mzee wa mji anayeitwa Herod,Leo au Fee katika movie hii anaamua kushindana nae katika kulengana risasi na bunduki, na katika mashindano hayo anafanikiwa kumjeruhi Herod shingoni lakini yeye anapoteza maisha.
Leo anakufa katika movie ya TOTAL ECLIPSE,Leo katika movie hii amaeigiza kama mwanashairi kutoka France anayeitwa Arthur Rimbaud  ambae anampenda kidume mwenzie anayeitwa Paul.         
 ANAKUFAJE? :Baada ya Leo au Arthur katika movie hii,kuona mahusiano yake na Paul yamevunjika anaamua kuondoka na kusafiri pande mbali mbali za dunia, anakuja kugundua kuwa ana cancer mguuni lakini kabla hajafanya operation ya kuukata inasambaa mwili mzima  na anakufa
 Leo anakufa katika movie ya ROMEO AND JULIETH,katika movie hii iliyotokana na vitabu vya mwanashairi maarufu William Shakespeare, Leo kaigiza kama Romeo kijana ambaye anampenda msichana Julieth lakini anapata wakati mgumu kuwa naye kutokana na ugomvi wa familia zao.     
ANAKUFAJE? : Leo au Romeo katika movie hii anakufa baada ya kumkuta mpenzi wake Julieth kanywa sumu, bila kujua kama sumu hiyo ni feki Romeo anaamu kunywa sumu halisi ili amfuate mpenzi wake, Julieth anaamka na kukuta tayari Romeo kanywa sumu na anakaribia kukata roho kwa uchungu anaamua kuchukua bastola na kujipiga kichwani hivyo wote Romeo na Julieth wanakufa.      
    Leo anakufa katika movie ya TITANIC, Katika movie hii Leo ameigiza kama kijana anayeitwa Jack baada ya kushinda tiketi katika kamaRi Jack anaingia katika meli ya Titanic na kukutana na mrembo Rose kwa pamoja wanafungua ukurasa wa mapenzi bila kujua nii kitawatokea mbeleni.
ANAKUFAJE? : Leo au Jack katika movie ya Titanic anakufa baada ya meli aliyekuwepo na mpenzi wake Jack kuzama na yeye kukosa boya la kuogelea  hivyo anakufa na baridi kali la maji ya kwenye bahari na kumuacha mpenzi wake Rose aliyefanikiwa kupata msaada.
Leo anakufa katika movie ya THE DEPARTED, Leo katika movie hii kaigiza kama  Bill Costigan ni police anayetakiwa aende undercover katika kundi moja la wahalifu wakati huo huo akihangaika kumtafuta mtu anayevujisha taarifa kutoka kwa polisi kwenda kwa wahalifu.
ANAKUFAJE? : Leo au Billy katika movie hii anakufa  baada ya kufanikiw kumkamata mtu anayevujisha taarifa za polisi kwa wahalifu anayeitwa Fink Colin katika harakati za kumkamata anajikuta akipigwa risasi ya kichwa na kufa hapo hapo.
 Leo anakufa katika movie ya BLOOD DIAMOND,Leo katika movie hii iliyoigizwa nchini Sierra Leone anaitwa Danny Archer jamaa anayefanya biashara za kimagendo akijaribu kusafirisha almasi ili afanikiwe kuondoka katika bara la Africa.almasi aliyokuwa nayo alipewa na Solomon ambae aliiba kwenye mgodi  na walihadiana na Archer kuwa atamsaidia kuonana na familia yake iliyopotea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.
ANAKUFAJE?: Leo au Archer katika movie hii anakufa baada ya kupigwa risasi akiwa katika harakati ya kuondoka Africa ili kwenda kuuza hiyo dhahabu,lakini kabla hajafa anamuachia Solomon na kumwambia akauze ili aweze kupata hela za kujisaidia yeye pamoja na familia yake.                      
Leo anakufa katika movie ya J.EDGAR,katika movie hii Leo ameigiza kama mkuu wa shirika la kijasusi la FBI anayeheshimika na kuogopwa kutokana na mchango wake katika nchi ya Marekani na alifanikiwa kupigana zaidi ya vita tatu na kufanya kazi na maraisi 8.                                              
ANAKUFAJE?: Leo kama kawaida yake anakufa tena katika movie hii lakini tofauti kidogo, humu wala hajapigwa risasi au kunywa sumu lakini Leo au J.Edgar anakufa baada ya kuzeeka na kuanza kushambuiwa na mardhi mara kwa mara na kuna siku anapata mshtuko wa moyo  na kudondoka hapo hapo.                                                                                                                                              
 Leo anakufa katika movie ya DJANGO UNCHAINED, Leo kaigiza kama Calvin Candie mtu ambaye ni tajiri na pia ni mbaguzi wa rangi, Calvin ana maadui wengi kutokana na utajiri wake na pia kummliki msichana mrembo Broomhilda kama mtumwa wake.
ALIKUFAJE? : Leo au Calvin katika movie hii anakufa baada ya kugundua kuwa Django na Dr King wanataka wamtoroshe mtumwa wake binti Broomhilda katika harakati za kuwazuia anapigwa risasi ya kifuani na kufa.
Leo anakufa katika movie ya THE GREAT GATSBY, Leo kaigiza kama Gatsby kijana maarufu na tajiri ambaye anaandaa party kila weekend katika nyumba yake kwa matumaini kuwa msichana anayempend Daisy atakuja kuudhuria moja ya party hizo ili aweze kurudiana nae kwa kuwa waliachana baada ya Daisy kuolewa na mtu mwingine na Gatsby kwenda vitani.
ANAKUFAJE? : Leo au Gatsby katika movie hii anakufa baada ya mume wa Daisy kugundua kuwa mkewe ana mahusiano na Gatsby, anaamua kufanya hila na kufanikiwa kumuua Gatsby kwa kumpiga risasi ya mgongo alipokuwa anaoga kwenye swimming pool.
 Hizo ni baadhi ya movies ambazo Leo kafa, ukimtoa Leo actors wanaongoza kufa wengine ni Bruce Willis, Sean Bean na John Hurt.Kwa upande wa Bollywood Shah Rukh Khan ndiye anayeongoza kufa katika movies nyingi.JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Betuel Edson

Author:

1 comment:

  1. Huyu Jamaa anavo penda kufa angekuwa mkorea angekuwa ni Jang Hyuk maana alikufa kwenye Iris akafa kwenye Slave Hunter

    ReplyDelete

Powered by Blogger.