LIST YA WAIGIZAJI WANAOWEZA KUVAA VIATU VYA WOLVERINE.

Mapema mwaka huu mwigizaji Hugh Jackman alitangaza rasmi kuachana na uhusika wa wolverine katika movies za X-MEN zitakazofuatia.Hugh Jackman alianza kuuvaa uhusika huo toka mwaka 2000 hivyo hadi leo ni miaka 17 imepita tangu auvae uhusika huo na kwa sasa ni muda muafaka kwa yeye kupumzika na kutoa nafasi kw waigizaji wengine.Hugh Jackman kathibitisha kuwa movie ya LOGAN ndio itakuwa ya mwisho kwake kama wolverine.Kampuni ya Marvel inayohusika na movie za X-men ina tabia ya kubadilisha waigizaji, kwa mfano uhusika wa Spider man umevaliwa na watu watatu kwa miaka tofauti tofauti pia uhusika wa Hulk umevaliwa na watu zaidi ya wawili,lakini Hugh Jackman ni mtu pekee  aliyeuvaa uhusika huu toka mwaka 2000 bila kubadilika.Mchakato wa kumtafuta mrithi wa Hugh Jackman katika uhusika wake wa Wolverine  unaendelea huku wadau mbali mbali wakitoa maoni yao kuhusu waigizaji gani wanaweza wakavaa uhusika huo vizuri.
Uhusika wa Wolverie unaangalia vitu vingi kama vile Muonekanano (ni vizuri ufuge udevu  kidogo),sauti na physique ya huyo mtu atakayevaa uhusika huo. Wafuatao ni baadhiya waigizaji wachache wanaoweza kuuvaaa uhusika wa Wolverine katika movies zijazo za MARVEL.
TOM HARDY, huyu jamaa naweza sema kuwa ndiye the right guy for the job, Tom Hardy ana swagger za kuwa Wolverine kabisaa, ana uwezo wa kuigiza soft guy katika movie moja na ukasema kuwa hawezi akaigiza kama tough guy katika movie nyingine, jamaa anajua kuuvaa uhusika na role ya Wolverine inamfaa kwa sababu uhusika huu unahitaji combination ya soft guy na tough guy kitu ambacho Tom Hardy anaweza akatuletea mezani. Mwangalie katika movie ya BATMAN DARK KNIGHT RISES alivyouvaa vyema uhusika wa BARNES pia mtazame katika movie ya MAD MAX: FURRY ROAD utakubali kuwa jamaa anajua.
Jinsi muonekano wa Tom Hardy utakavyokua kama akipewa uhusika wa Wolverine.
KEANU REEVES, Movies za huyu jamaa hazijawahi kutuacha salama, licha tu ya kuhusishwa na kuuvaa uhusika wa Wolverine Keanu alihusishwa pia kuuvaa uhusika wa Batman ambao baadae mwigizaji Ben Afleck alikuja kuuchukua. Keanu anafaa kabisa kuuvaa uhusika huu angalia movie kama MATRIX na JOHN WICK ndipo utajua kipaji halisi cha mwigizaji huyu.
SHAH RUKH KHAN, unaweza kushangaa kumuona mwigizaji toka Bollywood anahusishwa kuuvaa uhusika wa mwigizaji wa Hollywood, lakini Srk ni mmoja kati ya waigizaji wanaoweza kuvaa viatu hivyo. Kama sauti ya kibabe anayo kama unabisha anngalia movie ya RAEES, Udevu na muonekano wa ki-wolverine anao,na hata Hugh Jackman aliwahi kusema mtu ambae anaweza kumrithi ni Srk. Tatizo ni kuwa Srk katika miaka yake 25 ya uigizaji hajawahi kufanya kazi Hollywood hivyo itakuwa vigumu kwake kuaanza kuigiza Hollywood na kupewa uhusika mkubwa kama huo wa Wolverine.
Muonekano wa Srk katika movie y RAEES unavyofanana na muonekano wa Hugh Jackman katika movie ya WOLVERINE.
SCOTT ADKINS, Wengi tumemzoea kama BOYKA kupitia uhusika wake katika movie za UNDISPUTED,Scott ni mwigizaji anayeweza kuigiza tough na hata movie zake nyingi zipo hivyo lakini pia kuna baadhi ya movie kama SAVAGE DOG unaweza kumuona akiwa soft kidogo. Scott anaweza kuwa chaguo sahihi katika mchakato wa kumsaka mtu wa kuvaa viatu vya Hugh Jackman.
 KIT HARINGTON, YES winter is coming.....Kit Harington anafanya poa na series ya GAME OF THRONES amekuwa akihusishwa na wadau mbali mbali kama mrithi sahihi wa Hugh Jackaman.Tatizo ni moja Kit ni mwigizaji aliyezoea soft roles hata uhusika wake wa John Snow katika series ya G.O.T sio tough role kivile jambo linaloweza kumsumbua kidogo kama Marvel wakiamua kumpa uhusika huo.
kwa maoni yangu binafsi naona Kit Harington hafai kuwa Wolverine kama Marvel wakiwa na shida ya kumtafuta spider man mpya baada ya Tom Holland ( spider man wa sasa) basi Kit Harington apigiwe simu fasta kwa sababu uhusika huo unahitaji soft character kama yeye.
 SCOTT EASTWOOD, Mtoto wa mwigizaji Clint Eastwood bwana Scott naye anahusishwa mara kibao kuwa anaweza akawa Wolverine anayefuatia, Clint Eastwood na Tom Hardy ndio waigizaji wanaotajwa zaidi kuwania nafasi hii ya kuwa mrithi wa Wolverine.
Binafsi naona Scott hafai kabisa kuvaa uhusika wa Wolverine, Huyu jamaa ni mtoto wa mama kabisa hataweza kuwa tough kama Hugh Jackman, Mcheki alivyokuwa anaonewa na The rock kwenye THE FATE OF THE FURIOUS huyu jamaa anafaa kuigiza kama Prince katika movie kama CINDERELLA na sio kupewa uhusika kama Wolverine anaweza akawa kituko, naweza nisiwe sahihi sana kuhusu hili kwa sababu wadau wengi wameona anafaa lakini kwa mtazamo wangu kama mdau wa Movie naona jambo hili haliwezekani kabisa.
Hao ndio waigizaji wanaotajwa sana kuchukua mikoba ya Hugh Jackman lakini mwenye usemi wa mwisho ni kampuni ya Marvel ambayo inaweza kuchukua mmoja kati ya hao  actors hapo juu au wakamchagua wenyewe  watakayeona anafaa. Binafsi naona TOM HARDY ndiye mrithi sahihi kabisa wa Hugh Jackman na Marvel watafanya poa sana kama wakimchagua kuwa WOLVERINE mpya.


JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Betuel Edson

Author:

No comments

Powered by Blogger.