Mastar wanaochukiwa Hollywood.

Tyler Perry,anafahamika kupitia uhusika wake wa  ''Madea'', pia kasha-produce movies na series kibao kama ''IF LOVING YOU IS WRONG'' na ana mashabiki na mafaniko ya kutosha.
Sababu ya Kuchukiwa: Inadaiwa kuwa Tyler Perry huwa anapotosha jamii katika kuonyesha maisha ya mtu mweusi Marekani, Tyler katika movies anaonyesha kuna ubaguzi uliokithiri kitu ambacho kinafanya movies zake kupoteza mvuto kwani ubaguzi kweli upo ila sio kwa kiasi ambacho yeye anakionyeshana pia movies zake haziakisi maisha halisi anayoishi Mmarekani mweusi.
Zack Synder,Ni Director na Producer maarufu nchini Marekani,Movies kama 300 na Bat man Vs Superman ni baadhi ya kazi alizosimamia.
Sababu ya kuchukiwa:Kama ni mpenzi wa movie hakika huwezi kuusahua mwaka 2016 pale mashabiki wote dunia nzima walipokua wanasubiria movie ya BAT MAN vs SUPERMAN kwa hamu lakini kikaja kutokea kituko cha ajabu, movie hii ilipotoka iliwaangusha kabisa mashabiki wake kutokana na kuwa mbaya kupita kiasi hali iliyomfanya Zack aambulie matusi kutoka kwa mashabiki katika mitandao ya kijamii.
Shia LaBeouf, alikuwa maarufu sana kupitia mfululizo wa movies za TRANSFORMERS lakini baadae nyota yake ikafifia na akaanza kufanya mambo ya ajabu.
Sababu ya Kuchukiwa: Shia kalewa umaarufu na wala haeshimu mashabiki wake pia karibuni amekuwa ana kesi za ajabu ajabu hali iliyomsababishia kukamatwa na polisi mara kadhaa, aliwahi kwenda katika jumba la CINEMA akiwa na kibao kimeandikwa Am no longer famous pia aliwahi kukaa masaa kumi akitazama movies zote alizoigiza akidai anafanya majaribio.
Stacey Dash,Alifanya poa katika series ya CLUELESS na kujipatia mashabiki kibao.
Sababu ya kuchukiwa: Stacey mara kadhaaa katika interviews anaonekana ni mbaguzi wa rangi,aliwahi kusema chaneli ya B.E.T ifungiwe eti kwa sababu inagawa Tuzo kwa watu weusi pekee.
Billy Cosby,Alikuwa ni comedian anayependwa na kuheshimika Hollywood kupitia show yake ya The Cosby Show iliyokuwa inapendwa sana.
Sababu ya kuchukiwa: Anaripotiwa kuwa ni mnyanyasaji wa kijinsia na tayari wanawake zaidi ya 50 wamejitokeza wakidai kuwa Billy ameshawahi kuwanyanyasa kijinsia kwa mambo mengi kama vile kujaribu kuwabaka na kuwatomasa bila ridhaa yao.
MEL GIBSON, Bonge la Director akiwa kashatengeneza na kuziongoza movies kibao kama vile APOCALYPTO na movie ya YESU inayoitwa Passion of Christ.
Sababau ya kuchukiwa:Mel Gibson baada ya kuachana na Girlfriend wake anayeitwa Oksana alirekodiwa katika video akiwa anamtukana ex wake huyo matusi ya nguoni, huku akisema anataka ex wake huyo abakwe na kundi la watu weusi niggers,kauli yake haikuwafurahisha wengi kwa kuwa alikuwa ni actor anaonekana anajiheshimu hakuna mtu aliyefikiria kuwa ataongea pumba.
Harvey Weinstein, Ni Producer mwenye mafinikio makubwa sana kupitia movies kama PADDINGTON na WONDER WOMAN.
 Sababu ya kuchukiwa:Mwaka 2017 utakuwa mbaya sana kwake baada ya wanawake kibao maarufu Hollywood wakijitokeza na kusema kuwa aliwahi kuwanyanyasa kijinsia.Mastar kama vile Angelina Jolie na Salma Hayek wamethibitisha kuwa Harvey huwezi kupata nafasi katika movie yake bila kuombwa rushwa ya ngono.Na hivi karibuni Gal Gaggot mwanamama aliyeigiza katika movie ya WONDER WOMAN alitishia kujitoa katika kutengeneza WONDER WOMAN ya pili kama Harvey ataendelea kuwepo, kwa sababu alikuwepo katika Team iliyoandaa WONDER WOMAN part 1.
Adam Sandler,Comedian huyu kaonekana movies kibao kama vile COBBLER na CLICK.
Sababu ya kuchukiwa: Inasemekana kuwa Adam kapoteza radha na hachekeshi sana kama katika movies zake za zamani.
Anna Gunn,huyu hata hajafanya kosa ila anachukiwa tu kutokana na uhusika wake katika series ya BREAKING BAD katika show hii kaigiza kama mwanamke mwenye chuki sana dhidi ya mume wake,na kauvaa uhusika huu vizuri hadi watu wanahisi kuwa ni mkatili katika maisha halisia kama anavyoonekana katika uigizaji.
Stephen Collins,alifanya poa na series ya 7th HEAVEN akiiigiza kama baba mwenye upendo na watoto wake lakini inakuja kugundulika ni yupo tofauti kabisa na uhusika anaouvaa on screen.
Sababu ya kuchukiwa: Stephen ni kama Babu Seya wa Hollywood maana alikuwa na kesi ya kuwanyayasha kijinsia watoto wadogo na alikuja mwenyewe kukiri kuwa alikuwa na tabia hiyo lakini sikuizi ameiacha.

JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Betuel Edson

Author:

No comments

Powered by Blogger.