Sababu ya Kim Kardashian Kutozaa Mwenyewe Mtoto wake wa mwisho!


Baada ya habari kuzagaa kuwa Kim Kardashian na Kanye West wamepata mtoto wao mwingine wa kike, kupindia mitandao ya kijamii mashabiki wamekuwa na shauku ya kujua kwa nini Kim na Kanye wametumia Surrogacy/ au njia ya mtoto kutozaliwa na mama wa damu. Kim aelezea kila kitu kupitia tovuti yake juu ya kuzaliwa kwa mtoto huyo

Kim kaweka wazi kuwa alipata shida sana katika mimba mbili zilizopita. Katika post nyingine kupitia tovuti yake alisema "Preeclampsia na Placent accreta ni matatizo yanayomsumbua, kwa hiyo alipotaka kupata mtoto wa tatu, madaktari walisema sio salama kwake na mtoto kama angetaka kuzaa mwenyewe"

Kwa hiyo, ili wampate mtoto wao wa tatu, yeye na Kanye wakachua njia mbadala. Akelezea kuwa "Ingawa nimetumia neno surrogate hapo mwanzoni, ila gestational carrier ndo neno sahihi la kitaalamu kwa mwanamke anaebeba mimba ambayo hana uhusiano nayo"

Akielezea shida alizopata kihisia, alisema "Ni tofauti kabusa, wale watu wanaosema au kudhani kuwa hii ni njia rahisi basi wamekosea kabisa" akaongeza "Kwangu mie ilikuwa vigumu sana kutobeba mimba ya mtoto wangu, hasa pale ambapo nilibeba ya North na Saint"

Mwishoni akamalizia kwa maneno mazuri kidogo, "Sio kwa kila mtu, lakini kiukweli mimi nimempenda sana aliyebeba mimba ya mwanangu na hii ilikuwa ni moja ya vitu vizuri katika maisha yangu. Uhusiano na mwanetu umekuja fasta sana kama vile alikuwa nasi siku zote" akaongeza "Gestational Carrier wetu alikuwa special sana kwetu na kafanya ndoto yetu ya kupanua familia yetu kukamilika. Tunayo furaha kumkaribisha mtoto wetu wa kike nyumbani"

JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am a 2019 Digital Nomad from Tanzania

No comments

Powered by Blogger.