Apple Wataachia iPhone Inayokunjika Kufikia Mwaka 2020

A fan-made foldable iPhone concept

Moja ya makampuni ya teknolojia inayoongoza ambayo ni Apple inasemekana kuwa inafanyia kazi iPhone ya kipekee ambayo itakuwa na uwezo wa kukunjika nusu. Merrill Lynch wa Bankd Of Amerika aliwaambia CNBC kuwa Apple inashirikisha washirika wa Asia kuwa na simu inayoweza kukunjika na itaachiwa rasmi mwaka 2020.

Simu za kujikunja zinazoja kutoka Apple zimezungumzwa kwa miezi sasa, lakini inaonekana kampuni inafanya hatua kubwa zaidi. Lenovo na Samsung wamekuwa wakifanyia kazi juu ya wazo hilo lakini hakuna simu kama hiyo imejitokeza sokoni.

Katika habari nyingine za Apple, iPhone X Plus inasadikika kuachiwa hii Septemba na itakuwa na display ya OLED ya inchi 6.2, kubwa kwa simu yoyote ya iPhone hadi sasa.

JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am 21st century millennial with a passion of changing my hobby to a career

No comments

Powered by Blogger.