Tume ya Mawasiliano Marekani Yaruhusu Mpango wa Internet wa Elon Musk

SpaceX

Tume ya Mawasiliano marekani (FCC) leo imetoa leseni kwa SpaceX ya kurusha angani satelaiti za kutoa mtandao wa broadband, ikiashiria mara ya kwanza tume hiyo ya serikali imetoa ruhusa kwa huduma ya broadband ya low earth. Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa SpaceX Elon Musk amekuwa akizungumzia micro-satellite zake kwa ajili ya kutoa internet broadband kwa miaka kadhaa sasa, na mwaka 2017 kampuni ilianza kuharakisha juhudi zake kwa kukutana mara kwa mara na FCC na kuomba leseni ambayo itawawezesha kufanya kazi katika sehemu isiyoyotumiwa ya wigo wa broadband unaosimamiwa na FCC. SpaceX inapanga kuita huduma hiyo Starlink.

Mapema mwaka huu, SpaceX ilizindua satelaiti zake mbili za kwanza zilizopangwa kati ya satelaiti 12,000. Inaonekana kuwa kampuni inaanza na safu ya satelaiti 4,425, na FCC inahitaji angalau nusu ya satelaiti hizo zirushwe ndani ya miaka sita ijayo. "Kwa hatua hii, Tume inachukua hatua nyingine ili kuongeza upatikanaji wa high-speed broadband nchini Marekani," FCC ilisema katika taarifa kwa CNBC. SpaceX imepangwa kuanza kurusha satelaiti kwa ajili ya mtandao kuanzia mwaka ujao, wakati itakuja kichwa kwa kichwa na mtoa huduma mwingine wa mtandao, OneWeb.

"Tunashukuru uhakikisho wa FCC wa kina na idhini ya leseni ya kundi la satelaiti za SpaceX. Ingawa bado tuna mengi ya kufanya na kazi hii ngumu, hii ni hatua muhimu kuelekea nafasi ya SpaceX kujenga network ya satellite ya kizazi kinachofuata inayoweza kuunganisha dunia nzima na huduma  ya broadband yenye kuaminika na yenye gharama nafuu, hasa kufikia wale ambao bado hawajaunganishwa, "Gwynne Shotwell , Rais wa SpaceX na afisa wa uendeshaji mkuu, alisema katika taarifa iliyotolewa kwa The Verge. SpaceX inatarajia Starlink inaweza ingiza kipato kikubwa sana ambacho kinaweza kusaidia kukabiliana na R & D na gharama za uendeshaji wa kampuni hiyo ya roketi. Makadirio ya kifedha, yaliyofanywa na Wall Street Journal mwaka jana, yalionyesha SpaceX inatarajia zaidi ya subscribers milioni 40 wa Starlink kufikia mwaka 2025, sawa na dola bilioni 30 katika mapato.JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am 21st century millennial with a passion of changing my hobby to a career

No comments

Powered by Blogger.