Raisi wa PSG Adai Kutopendezwa na Njia za Frolentino PerezRaisi wa Club ya Paris Saint Germain Nasser al-Khelaifi ameweza kuweka bayana kuwa against na njia ambazo club ya Real Madrid ilitumia kumfukuzia mchezaji wa club hiyo Neymar Jr.

Club hiyo ya Real Madrid imekuwa ikijaribu kwa muda sasa kuweza kumsajili mchezaji huyo wa Kibrazil, na club hiyo, Na iliweza kutoa taarifa mara kazaa kuwa usajili wa mchezaji huyo upo mbioni kukamilika.

Raisi wa PSG aliweza kuongea wakati wa uzinduzi rasmi wa partnership na Michael Jordan kupitia kampuni ya Nike, alionge na jarida maarufu la Marca kuwa "Kiharisia inaumiza sababu sio fair kwa mtu au club nyingine kuongea na mchezaji wetu. Hatukupenda kabisa na tuliweza kuongea hili na Real Madrid. Tuna mahusiano mazuri na wamekuwa wakidai wanatuheshimu naimani ni kweli."

"Tunaiheshimu Real Madrid pamoja na Raisi wake Frolentino Perez, ila nafikiri ni muhimu kwa kila mmoja kama hatutofanya kazi nyuma ya migongo...sijui kama umenielewa."

Neymar alijiunga na club ya PSG akitokea Barcelona August mwaka jana na kuweza kuandika rekodi ya kuwa mchezaji ghari zaidi duniani.


JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Mwamlima Peter

Author:

No comments

Powered by Blogger.