UFC: Conor McGregor Asifiwa Pamoja Na Kushindwa Dhidi ya Khabib Nurmagomedov

Image: GETTY
Tarehe 7, Octoba McGregor alirudi UFC baada ya karibu miaka miwili ya kuwa nje ya ulingo lakini amepigwa na Mrusi huko Las Vegas.

Pambano hilo lilikuwa ni mchuano wa UFC Lightweight lakini McGregor alipigwa katika 'round' ya nne.

Na ingawa McGregor alitolewa na Khabib ambaye wengi wanamuita "Aisiyepigika", Bingwa wa sasa wa UFC Featherweight Max Holloway anaamini kwamba Conor alifanya vizuri zaidi katika pambano hilo licha ya kupigwa round ya nne.

“Conor alifanya mambo mengi makubwa ndani ya pambano” Holloway alisema.

“Kiukweli jamaa alishinda round ya tatu ingawa Khabib nae alifanya mambo makubwa pia.

“Khabib alikuwa hatua moja mbele, inchi moja mbele. Khabib akikukamata, yaani huwa anawafanya watu waonekane kama midoli ya watoto.

“Siwezi sema Conor alionekana kama mdoli, kila alichofanya kilikuwa ni sahihi kabisa, lakini kosa moja na Khabib akaitumia nafasi hiyo.”

Pambano hilo la 229 la UFC litakumbukwa siku zote hasa baada ya kuleta ugomvi mkubwa kati ya timu ya Conor na Khabib. Mara tu baada ya Khabib kutajwa mshindi, mrusi huyo aliruka wigo wa ulingo na kujaribu kumshambulia Dillon Danis ambae ni mmoja kati ya wanakikundi cha Conor.

Hata wafuasi wa Khabib walimshambulia Conor McGregor akiwa ndani ya ulingo na hapo ndipo mzozo mkubwa ukazuka

Cha kushangaza zaidi, hata Floyd Mayweather aonyesha kutopendezwa na ushindi wa Khabib
“ Simtambui huyo jamaa Mcgregor alikuwa akipambana nae, lakini najua huyo jamaa alikuwa anapambana na mtu mashuhuri aiyepigika” Alisema Mayweather. Hiyo iko wazi kwa maneno hayo anamsifia ConorJIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am 21st century millennial with a passion of changing my hobby to a career

No comments

Powered by Blogger.