Triple H: Afanyiwa Upasuaji Hospitali Baada ya Kujeruhiwa Vibaya Ulingoni


Mwanamieleka wa WWE, Triple H alirudi ulingoni kwa mara nyingine wiki iliyopita kwenye pambano la WWE la Crown Jewel PPV huko Saudi Arabia, ambako alikuwa timu moja na ndugu yake wa siku zote Shawn Michael katika mechi ya timu dhidi ya The Undertaker na Kane. Wakati DX alihakikisha unapatikana ushindi dhidi ya The Brothers of Destruction, Triple H hakuwa na bahati ya kutosha kutoka ulingoni akiwa safi afya.
Mwishoni mwa mechi, H alichanika misuli yake ya pectoral ingawa alikuwa na uwezo wa kumaliza show ndio maana akashindwa kuendelea na ziara ya WWE Uingereza. Badala yake, The Game alirejea Marekani kupata matibabu -JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am a 2019 Digital Nomad from Tanzania

No comments

Powered by Blogger.