YouTuber 'MrBeast' Maarufu Kwa Kugawa Pesa Aeleza Wapi Anatoa pesa hizo


Jimmy "MrBast" Donaldson aliyejitengenezea jina kwenye YouTube kwa kutoa zaidi ya dola milioni kwa watu tu mitaani na marafiki. Sasa, video yake mpya kwenye channel yake inajibu swali ambalo anapata mara nyingi kutoka kwa mashabiki: fedha zote zinatoka wapi?


Misaada ya dola milioni 1 ya Donaldson inatoka kwa mikataba na brands, lakini pia hutegemea video ijizolee umaarufu ili hata yeye ajipatie mapato yake binafsi. Yeye anapozidi kuwa maarufu, ndivyo brands nyingi zinataka kufanya kazi naye, na ndivyo zaidi anapata mapato toka AdSense. 


Ilianza na mkataba aliyofadhiliwa na makampuni kama Quid, kwenye video za $ 10,000. Donaldson alitoa karibu kila kitu kwa watu: watu wasiokuwa na makazi, Wachezaji wa magemu wa Twitch, wazazi wake, marafiki zake, na hata wafuasi wake. 


Donaldson aliweza kuikuza channel yake na kuvutia wafuasi zaidi ya milioni 5 katika mtandao wa YouTube, video zake nyingi hupata views zaidi ya milioni 10 ndani ya wiki chache tu, hivyo unaweza pata picha ni kiasi gani cha pesa anaingiza.


"Ikiwa unataka siri, ikiwa unataka kujua wapi pesa zanatoka - wazazi wangu sio matajiri, nina umri wa miaka 20 tu, kila dola ninayoingiza imetoka YouTube, na YouTube hulipa vizuri zaidi ya unavyofikiri, "Donaldson alisema.

JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am a 2019 Digital Nomad from Tanzania

No comments

Powered by Blogger.