Cr 7 KUWASILISHA DNA KWA POLISIMchezaji nguli duniani anayekipiga katika klabu ya Juventus kwa sasa, Cristiano Ronaldo almaarufu Cr 7, ametakiwa kuwasilisha vipimo vya vinasaba (DNA) kwa polisi ikiwa ni mchakato wa kuisaidia polisi kufanya uchunguzi wake katika sakata linamuhusu la ubakaji.
Mchezaji huyo raia wa Ureno anatuhumiwa kwa kesi ya ubakaji iliyoripotiwa na mwanadada Kathryn Mayorga. Kathryn alifungua kesi hiyo akimtuhumu Cr 7 kumbaka mwaka 2009 kipindi ambacho hakuweza kumtambua mchezaji huyo kwa jina.
Mwanadada huyo ameomba shauri lake kufunguliwa upya ambapo Cr 7 ametakiwa kuwasilisha vipimo hivyo vya vinasaba kama sehemu ya uchunguzi kuhsiana na kesi inayomkabili. Kathryn Mayorga amekiri kufanyiwa kitendo hicho na kusema kwamba alipewa kiasi cha $375k kama namna ya kumnyamazisha kuhusu tuio hilo.
 Polisi wamethibitisha kufanya uchunguzi juu ya sakata hilo na kukiri kumtaka Cr 7 kuwasilisha vinasaba (DNA). Wakati hayo yote yakiendelea, mchezaji huyo amekana kuhusika na kesi inaymkabili na amekubali kutoa ushirikiano kwa polisi kudhihirisha kutohusika kwake na kesi hiyo.

JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Ayoub Nyangasi

Author:

I am creative in all aspects

No comments

Powered by Blogger.