Cristiano Ronaldo akanusha sauti zilizorekodiwa kumtuhumu kuwa na mpenzi wa siri

Star wa soka wa club ya Juventus Cristiano Ronaldo amekanusha tuhuma zinazomkabili kuhusiana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa siri na mwanamitindo Jasmine Lennard. Ikumbukwe kuwa mwanadada Jasmine ambaye ni nyota wa UK "Celebrity Big Brother" alitangaza wiki hii kupitia mitandao ya kijamii kuwa amewahi kuwa na mahusiano na Cristiano Ronaldo mara kadhaa kwa siri. 
Jasmine alipost sauti amabzo alidai ni za Cristiano Ronaldo alimrekodi wakati akimfanyia matendo kadhaa ya unyanyasaji kwa kumkalipia na kumtishia.

Licha ya tuhuma hizo, watu waliokaribu na mchezaji huyo wamekanusha kwa kusema Cristiano hajawahi kuwa karibu na mwanamitindo huyo wala hajawahi kukutana nae.
 "hajawahi kuwa na mahusiano naye wala kuwahi kukutana nae kwa kipindi cha miezi 18 kama ambavyo Jasmine anadai" walisema watu wa karibu na Cristiano. Waliongeza pia
"Sauti zilizopostiwa na Jasmine Lennard kwenye mitandao ya kijamii sio ya Cristiano Ronaldo, na tumejianga kuchukua hatua za kisheria dhidi yake"
Jasmine alifuta account yake ya Twitter muda mfupi baada ya kupost sauti hizo.
JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Ayoub Nyangasi

Author:

I am creative in all aspects

No comments

Powered by Blogger.