Kevin Hart Aliambiwa Hawezi Kuchekesha, Atafute Kazi Nyingine!


Kevin Hart ni mojawapo ya wachekeshaji wenye mafanikio makubwa na mmoja wa watu maarufu ambao hulipwa donge nono zaidi nchini Marekani.

Lakini Hart hakuwahimiza mara zote watu kucheka na kupiga makofi. Kwa kweli, anakumbuka wakati mmoja muhimu katika kazi yake ya uchekeshaji, wakati mtu mmoja muhimu katika ulimwengu wa comedy alimwambia aache kuchekesha atafute kazi nyingine.

Hart anakumbuka maoni aliyopata kipindi anaanza uchekeshaji kutoka kwa Lucien Hold, comedy club talent booker na meneja anayejulikana kwa kugundua vipaji vya wacheshi kama Eddie Murphy, Chris Rock na Jerry Seinfeld, na wengine kibao.

"Ikiwa huyu jamaa anasema wewe unachekesha, basi jua kweli unachekesha," Hart anasema. "Ikiwa mtu huyu anasema una kipaji, kweli ulikuwa nacho. Na nilifanya kazi kwa bidii ili nimfikie mtu huyu, na nikamwendea."

Lakini matokeo hayakuwa yale aliyotarajia.

"Nilichekesha mbele yake, naye akaniambia mbele ya uso wangu kwamba ninapaswa kufikiria juu ya kupata kazi nyingine," Hart anasema. "Aliniambia mbele ya uso wangu kwamba anahisi ucheshi sio kitu chake".

Hart anakumbuka kwamba ilikuwa ni pigo kubwa katika maisha yake, na alikaa mda mrefu akifikirie achukue uamuzi gani baada ya kusikia maneno yale.

Hapo alijifunza somo muhimu pia: "Kila mtu atakuwa na maoni, kila mtu atakuwa na kitu ambacho wanaweza kusema, lakini hatua yako inategemea mapenzi yako juu ya kile unataka," Hart anasema.

"Basi kama unaweza kuamka na kusonga tu, vila kuacha, basi utakuwa poa. Unaporuhusu wengine kuamuru harakati zako, basi utakuwa unaathiriwa kila wakati."

Kevin Hart kaumaliza mwaka 2018 kwa kishindo kikubwa, mara baada ya Forbes kumweka nafasi ya pili kati ya "highest-paid comedian in the world in 2018" akiwa chini kidogo ya Jerry Seinfeld
JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am a 2019 Digital Nomad from Tanzania

No comments

Powered by Blogger.