Mauzo ya Apple Yaathiriwa na "Ubadilishaji Nafuu wa Betri za iPhones"


CEO Tim Cook wa Apple ametoa barua kwa wawekezaji wake ikiweka wazi kuwa wanatarajia kupoteza dola bilioni 9 ya mapato kwa sababu ya mahitaji dhaifu ya iPhone ambayo kwa sehemu kubwa husababishwa na watu wengi kubadilisha  betri za iPhones zao, kulingana na barua iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji Tim Cook kuongea kwa wawekezaji.

Mwaka jana, Apple ilikubali kuwa imekuwa ikipunguza spidi ya model za zamani za iPhones ili kupunguza uwezekano wa kuharibika kwa betri zake kitu ambacho kilisababisha model hizo za simu kujizima zenyewe baada ya kutumika na kupata moto. Baada ya kukubali dai hilo la kupunguza spidi kwa simu hizo basi wakatoa ofa ya kupunguza ada ya ubadilishaji wa betri toka $79 hadi $29 kama njia ya kuwaomba msamaha wateja wake.

Kupungua kwa ada ya kubadilisha betri ilimaanisha kuwa watu wengi mwaka 2018 walichofanya ni kubadilisha betri tu - badala ya kununua model za hivi karibuni za iPhone. Kwa kuwa betri za iPhone ni nafuu na rahisi kuchukua, watu wachache wananunua iPhones mpya ambazo gharama yake inafikia hadi $ 1,449. JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am a 2019 Digital Nomad from Tanzania

No comments

Powered by Blogger.