MISS UNIVERSE KACHUMBIWA


Mrimbwende wa dunia mwaka 2017 Demi Leigh Nel Peters amechumbiwa na Tim Tebow baada ya wawili hao kuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kadhaa. Hayo yamethibika mara baada ya Tim Tebow kupost kwenye ukurasa wake akimshukuru mrembo huyo kwa kukubali ombi lake. Maneno ya Tim yalisomeka
"Thank you for saying Yes and making me the happiest man in the world" akimaanisha "ahsante kwa kusema ndio na kunifanya mwanaume mwenye furaha duniani". Tim hakuishia hapo aliendelea kwa kusema " You’re the love of my life, and I can’t wait to spend the rest of my life with you." Akimaanisha " wewe ndiye mpenzi wa maisha yangu, siwezi kusubiri kuishi nawe kipindi chote cha maisha yangu. 
Kuthibitsha mahusiano yao, mlimbwende huyo wa dunia wa mwaka 2017 hakuwa mbali kwani alimjibu Tim kwa kucomment maneno yaliyosomeka " Any dreams I’ve ever had, you’ve exceeded them all! I love you and I can’t wait to spend forever with you!"
Ifahamike kwamba Demi Leigh, ni mshindi wa taji la miss Universe 2017, ana umri wa miaka 23 na raia wa Afrika Kusini. Leigh ameonekana Florida Marekani akiwa na mchumba wake huyo mpya kwa msimu wote wa sikukuu. JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Ayoub Nyangasi

Author:

I am creative in all aspects

No comments

Powered by Blogger.