Saa za Mayweather zazua gumzo

 
 Mwanamasumbwi wa Kimarekani " Floyd Mayweather" ameonesha idadi ya saa za gharama anazomiliki kwa sasa. Licha ya kuwa na saa zipatazo 41, Floyd ameweka wazi juu ya saa yake ya gharama zaidi yenye thamani ya kiasi cha $ 18 millioni ambayo aliita "one and only", akimaanisha yake ya pekee.
Inasemekana Floyd aliamka akiwa na furaha sana kiasi kwamba akaamua kufanya live video akionesha baadhi ya briefcase zake anazotumia kutunza saa. Ameonesha saa hizo huku akisema maneno ya kujinadi kuhusiana na saa za gharama anazomiliki. 

Saa hiyo yenye gharama ya $ 18 millioni inayofahamika kwa jina la " THE BILLIONAIRE WATCH" imetengenezwa na Jacob company mwaka 2015. Floyd amesema alinunua saa hiyo iliyosheheni madini ya Almasi kutoka kwa Sonara wa Kijapani aitwaye Tadashi Fukushima. Mara baada ya kununua saa hiyo Floyd amekiri kuwa hajanunua tena kito cha thamani mpka leo. Ifahamike kuwa Floyd alitengeneza pesa nyingi sana kwa uwezo wake wa kupambana ulingoni. Na moja kati ya mapambano ambayo yalimpa pesa nyingi ni pamoja na pambano dhidi ya Man Pacquia kiasi cha $300 mil, na pambano dhidi ya Mcgregor kiasi cha $300 mil.
 Kutokana na kuingiza pesa nyingi kupitia mapambano yake, Mayweather amesema hatoshindwa kununua saa nyingine yoyote ya gharama atakayoipenda.
JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Ayoub Nyangasi

Author:

I am creative in all aspects

No comments

Powered by Blogger.