Nigeria: Aliko Dangote Yupo Kwenye Hatari ya Kupitwa Utajiri na Adenuga - 2019 Forbes


Tycoon wa Biashara, Alhaji Aliko Dangote, anaweza akawa bado anashikilia nafasi yake kama tajiri anaeongoza Afrika akiwa na thamani ya dola 10.3bn, akifuatiwa karibu na Mwenyekiti wa Globacom, Mike Adenuga ($ 9.2bn), lakini kulingana na orodha ya hivi karibuni ya Forbes, utajiri wa Dangote umeshuka kwa $ 2.1bn toka mwaka 2018. Utajiri wa Aliko Dangote Mwaka 2015, uliripotiwa kuwa dola 25bn, lakini miaka mitatu baadaye, fungu hilo limepungua kwa dola 15bn.


Mike Adenuga

Wanaijeria hawajaonyesha kuridhika na makadirio ya utajiri wa Dangote, kutoridhika kumekuja baada ya Mike Adenuga ambae pia ni kutoka Nigeria kuonekana akimkaribia Dangote kwa kasi ya ajabu.
Hii inaonyesha wazi kuwa Wanaijeria hawako tayari kushuhudia Dangote akishuka chini. Kulingana na Forbes wenyewe, wanadai utajiri wa Adenuga ulitoka $5.3 billion januari mwaka 2018 . hadi $9,2 billion kwa kuwa Adenuga ametoa nyaraka na maelezo zaidi juu ya mali zake.

Je, Tuandae Episode 43 ya Mambo Kumi Kuhusu Aliko Dangote?

JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am a 2019 Digital Nomad from Tanzania

No comments

Powered by Blogger.