Nokia Inatarajiwa Kuja na Simu Yenye Kamera Tano nyuma!


Kwa zaidi ya mwezi sasa kuna video imekuwa ikivuja mitandaoni ikionyesha simu ya Nokia ikiwa na kamera tano, lakini video mpya inaonyesha kuwa simu hiyo inaweza kuachiwa rasmi hivi karibuni. Evan Blass kwanza aliweka picha ya Nokia 9 PureView kwenye mtandao wake wa Twitter mapema jana, na sasa mysmartprice imechapisha kile kinachoonekana kama ni video ya kutambulisha rasmi.

Nokia 9 PureView inaonekana sawa na Nokia 8 Sirocco, isipokuwa kwa nyuma. Video hii inaonyesha penta-lens inayoweza kupiga picha tano kwa mpigo na madai ya ufanisi bora katika mazingira ya mwanga hafifu. Mysmartprice inaripoti kwamba Nokia 9 PureView pia itatumia Qualcomm Snapdragon 845, 6GB ya RAM, na 128GB nafasi ya kuhifadhi.

HMD ilichukua brand ya PureView kutoka Microsoft mapema mwaka jana, na kushirikiana na Zeiss ili kuunda Nokia za Android. 

JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am a 2019 Digital Nomad from Tanzania

No comments

Powered by Blogger.