Wajanja wanatumia Drones kupiga selfie


Kwa miaka ya karibuni kumezuka mtindo mpya wa kujipiga picha unaojulikana kama "selfie". Watu wengi wamekuwa wakipambana kununua simu zenye uwezo mkubwa wa camera ilimradi kutimiza matakwa yao ya kupata selfie kali. Wapo waliodiriki hata kutumia kamera kubwa na kujaribu kupiga picha hizi za selfie. Hali hii ilimfanya kila mmoja kujaribu kupata selfie ya kipekee ambayo ingewastaajabisha na kuwavutia wengi mitandaoni kiasi kwamba ikapelekea ubunifu wa selfie stick. Selfie stick zilitumika kupiga picha katika elevation angle na kunogesha picha hizi zaidi.

 Mambo  yamebadilika kwa sasa kwani imeletwa technolojia mpya ya Drones ndogo kwa ajili ya kupiga selfie. Haikichukua muda mrefu sana kabla ya wagunduzi hawa kufanya maamuzi ya kuleta drones ilimradi wanahakikisha zinapatikana selfie nzuri zaidi.

Ni kitu gani hiki?
Hii ni aina mpya ya drone inayofahamika kama Drone X Pro, iliyobuniwa kuhakikisha inaboresha upigaji wa selfie toka angle za mbali na zenye ubora zaidi kulingana na matakwa ya wapiga selfie. Licha ya kuwa zimekuja kuuwa soko la selfie stick, selfie drones zimeonekana kupendwa zaidi kutokana na uwezo wake wa kwenda mbali , wepesi kubebeka na urahisi wa kutumia.

Ni fursa mpya kwa wapenda selfie kupata drones ili kuhakikisha wanapiga picha zitakazoushangaza ulimwengu kwa ubora wa selfie. Je uko tayari kutumia hizi kama mbadala wa selfie stick?JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Ayoub Nyangasi

Author:

I am creative in all aspects

No comments

Powered by Blogger.