YouTube Ilishushwa Chini Kwa Lisaa Leo


YouTube ilikuwa chini kwa saa na nusu leo, na kusababisha watazamaji na creators ulimwenguni kote kushindwa kutazama na kupakia video.

Tatizo hilo lilionekana kuanza saa 5:10 usiku na tatizo hilo likaja kupata utatuzi saa 7 kasoro robo usiku.

"Ikiwa YouTube haionekani kwako au unaona ujumbe wa error katika tovuti - tuko tunashughulikia," akaunti ya usaidizi wa kampuni hiyo ilitangaza leo usiku baada ya tatizo hilo kutokea

Tofauti na balaa kubwa zaidi lililotokea YouTube mnamo Oktoba 2018, ambapo kila mtu aliathiriwa kwa masaa machache, inaonekana kama hali hii iliyotokea leo iliathiri watumiaji wachache tu.

Mmoja wa watu walioathiriwa na tatizo hilo ni MrBeast, YouTuber Maarufu.
"Nilikuwa nikipakia video lakini YouTube imeshuka," Jimmy "MrBast" Donaldson, mwenye subscribers zaidi ya milioni 5, aliandika tweet.

RELATED: YouTuber 'MrBeast' Maarufu Kwa Kugawa Pesa Aeleza Wapi Anatoa pesa hizo
JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Jimmy James

Author:

I am a 2019 Digital Nomad from Tanzania

No comments

Powered by Blogger.