Callum Hudson Odoi Kukabiziwa Jezi #10 ya Hazard
Mabingwa Europa kwa msimu wa 2018/19 Chelsea Fc imempa ofa ya mkataba mpya msambuliaji na winger wake Callum Hudson Odoi.

Kabla ya kusaini mkataba huo Callum Hudson Odoi amedai kuwa anataka kufahamu kuwa ataweza kucheza muda mwingi zaidi kuliko hapo nyuma. Winger huyo mwenye miaka 18 alikuwa anawindwa na club ya Buyern na alikuwa tayari kujiunga na mabingwa hao wa Germany.

Maongezi sasa yanaendelea vizuri kwa winger huyo ambaye anamkataba wa mwaka mmoja na The Blues ameweza kupewa namba 10 ambayo ilikuwa inavaliwa na Eden Hazard.
Jarida la the Sun limeeleza kuwa winger uyo huwenda akabakia klabuni hapo kwani inaaminika hata Sarri anaondoka msimu kwenda kuitumikia Juventus.


JIUNGE NA NEWZFID SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za burudani kimataifa! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Newzfid!
Mwamlima Peter

Author:

No comments

Powered by Blogger.